|
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA ATHUMANI DIWANI ENEO LA
TUKIO |
|
WANAKIJIJI
ISENGO IZIWA WAKIWASIKILIZA WANAUSALAMA HUKU WAKIWA NA SIRAHA ZAO ZA
JADI |
|
CHANZO
CHA MAJI IZIWA |
|
MAMA
WA KISAFWA AKIWA AMEFICHA PANGA |
|
SIRAHA
ZA JADI ZILIZOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
MNAMO TAREHE
28.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS MAAFISA WA HIFADHI YA MALIASILI NA UTALII
WAKIONGOZWA NA MENEJA WA HIFADHI HIYO KASMIR S/O NGOWI NA AFISA MISITU WA JIJI
LYOWA S/O WAYANGA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA WALIFIKA
KATIKA MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA KWA AJILI YA KUENDELEA NA OPERESHENI YAO YA
KUWAONDOA WATU WALIOVAMIA NA KULIMA NDANI YA HIFADHI YA SAFU YA MLIMA MBEYA
[MBEYA RANGE FOREST RESERVE] ENEO AMBALO NI CHANZO CHA MAJI NA VIUMBE HAI ZOEZI
LILILOANZA TANGU TAREHE 28.12.2012.
HATA HIVYO KABLA
ZOEZI HILO KUANZA KUNDI KUBWA LA WANANCHI WA ENEO HILO WAPATAO 400 WAKIWA NA
SILAHA ZA JADI WALIFIKA ENEO HILO WAKIWA WAMEJIANDAA KUFANYA VURUGU
WAKISHINIKIZA KUTOFANYIKA KWA ZOEZI HILO. KATIKA VURUGU NDOGO ILIYOTOKEA YOHANA
S/O MDEWA,MIAKA 54,MSAFWA,MWANACHAMA WA ASASI YA KIRAIA YA KUTUNZA
MAZINGIRA MKAZI WA KIJIJI CHA IHOMBE , ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI ,
WAKIDAI NDIYE MSALITI ALIYEWALETA WATU HAO ,HIVYO POLISI WALIMUOKOA NA
KUMHIFADHI KATIKA OFISI YA MTENDAJI KATA.
PIA KATIKA VURUGU
HIZO KULITOKEA UHARIBIFU KATIKA GARI STJ 1830 MALI YA WAKALA WA HIFADHI YA
MISITU NYANDA ZA JUU KUSINI KWA KUPASUKA WIND SCREEN YA MBELE NA SIGHT MIRROR YA
KUSHOTO NA MAGARI MENGINE YA IDARA HIYO STJ 1821 NA STJ 1832 KURUSHIWA MAWE
PIA KUBOMOA MADARAJA MAWILI YALIYOPO KIJIJINI HAPO. KUFUATIA HALI HIYO KIKOSI
CHA KUTULIZA GHASIA MKOA WA MBEYA WALIFIKA ENEO HILO HATA HIVYO WANANCHI
WALITAWANYIKA KWA KUKIMBIA. POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA ENEO HILO
WALITOA WITO KWA WANANCHI KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI AMBAPO WALIKIRI NA KUDAI
HAWAKUELEZWA JUU YA ZOEZI HILO NA WAMEAHIDI KUJENGA WAO WENYEWE MADARAJA
WALIYOKUWA WAMEBOMOA.
UONGOZI WA SERIKALI
YA WILAYA YA MBEYA CHINI YA MKUU WA WILAYA DR NORMAN SIGALA NA MSTAHIKI MEYA WA
JIJI ATHANAS KAPUNGA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO MHE DIWANI NA MTENDAJI KATA
YA IZIWA KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA BAADAE WAMEKUBALIANA KUWA WATU WOTE
WALIOVAMIA ENEO HILO WAHAKIKISHE WAMEHAMA KABLA YA MWEZI AGOST – 2013. KWA SASA
HALI IMEREJEA KUWA SHWARI KIJIJINI HAPO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO
KUSHURUTISHWA. PIA ANAZIDIKUSISITIZA KUWA MAZUNGUMZO NDIO NJIA MUHIMU NA SAHIHI
YA KUWASILISHA MALALAMIKO/KERO BADALA YA FUJO NA VURUGU ZISIZOKUWA NA TIJA KWANI
ZINAWEZA KULETA MADHARA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO. KAMANDA AMEAHIDI KUWA
WALIOVUNJA SHERIA KWA KUMJERUHI YOHANA S/O MDEWA NA KUFANYA UHARIBIFU WA
MADARAJA WATAFUATILIWA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
|
on Tuesday, January 29, 2013
Post a Comment