|
Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel
Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai
kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
|
|
Sabina Lameck mke wa mchungaji anaedaiwa kuaachwa sababu
ya uchawi |
|
Katikati mama mzazi wa mchungaji Elia Jongo wakiwa katika
kikao hicho |
|
Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa makini kusikiliza kisa
hicho |
|
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa
sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane
na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi
anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo. ambaye alikuwa mke wa mchungaji
Elia
|
|
Huyu ndiye muumini wa kanisa hilo anayedaiwa kutaka
kuolewa na mchungaji Elia pia muumini huyu ni mzee wa kanisa
hilo |
|
Mchungaji elia na dada yake wakiwa makini kumsikiliza
mchawi wake |
|
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane
alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani nayeye
kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema
mchungaji huyo kwa
hasira.
|
|
Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana kwa jina moja la
Pasta Lugito |
|
Hili ndilo kanisa la Calnel Centre mbeya lipo katibu na
kiwanja cha ndege mwanjelwa Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel
Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai
kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi katika kanisa hilo
lililopo Airport Jijijini Mbeya baada ya Mchungaji huyo kupokea ujumbe mfupi
katika simu yake ya mkononi kutoka kwa Mwanamke anayedai alikutwa mke wake
ambaye waliachana miaka mine iliyopita.
Mchungaji huyo akiwa mbele ya wazee wa kanisa, Familia
yake, waumini pamoja na wanahabari alisema sababu ya kuwakusanya watu hao
kumetokana na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Sabina Lameck akitaka
kutubu kwa mabaya aliyomtendea mumewe.
Hata hivyo baada ya mwanamke huyo kupewa nafasi ya kuanza
kujieleza alianza kumtuhumu muumini wa kanisa hilo kuwa anauhusiano na mchungaji
ambaye ni mumewe wa ndoa ambapo pia alidai kuwa mwanamke huyo alichukua nguo za
mchngaji na mkewe kwa madai ya kupeleka kwa mganga ili kusudi awasaidie
warudiane.
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa
sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane
na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi
anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo.
Kwa upande wake mchungaji Jongo alimtuhumu mwanamke huyo
kuwa ni mshirikina na kwamba sababu ya kutengana naye ni kutokana na mwanamke
huyo kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa hali aliyosema alidhalilishwa kama
mchungaji.
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane
alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani nayeye
kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema
mchungaji huyo na kuongeza.
“ amekuja leo hapa baada ya kusikia mimi nataka kuoa
muumini wangu ambapo yeye ameanza kumzushia kuwa ni mshirikiana kitu ambacho si
cha kweli lakini kama kuna ukweli wowote utajulikana kwa sababu Mungu yupo,”
alisisitiza Mchungaji huyo.
Hata hivyo usuluhishi huo haukufika mwafaka baada ya
kuibuka kwa malumbano hali iliyomlazimu msimamizi wa usuluhisho huo Askofu wa
kanisha hilo laiyejulikana kwa jina moja la Pasta Lugito kuahilsha mazungumzo
hayo huku wakimpiga marufuku mwanamke huyo kukanyaga katika makazi ya
mchungaji.
Picha na Mbeya yetu
|
on Wednesday, January 30, 2013
Post a Comment