Mbunge wa Bukoba Mjini (Waziri wa Maliasili na Utalii) Mh. Balozi Hamis Kagasheki
*************
Kwa
habari tulizotumiwa na mdau wetu kutoka Bukoba zinesema mgogoro huo
kati ya Mbunge wa Bukoba Mjini na pia ni waziri wa Maliasili na Utalii
Mh. Balozi Hamis Kagasheki ameingia kwenye mgogoro na Meya wa Bukoba
Mjini Mh. Anathory Amani kwasababu ya suala la ubomoaji wa soko kuu la
hapo Bukoba Mjini. Meya wa huyo anashinikiza soko livunjwe na kujengwa
la kisasa lakini mbunge wa jimbo ilo na baadhi ya madiwani
hawakubaliani na suala hilo kwani hajajulukana hatma ya wafanyabiashara
wa soko hilo la Bukoba.
Hili
suala lilisababisha madiwani wawili wanaoziwakilisha kata mbili ndani
ya Manispaa ya Bukoba walitembezeana mkono baada ya kutokea mabishano
katika kikao cha maadili chenye lengo la kumshinikiza Mh. Meya Anathory
Amani ajiuzuru.
Madiwani
hao waliopeana kichapo na kuzua taflani kubwa hadi kufikishwa kituo cha
polisi ni Diwani wa Kata ya Kahororo Mh. Chief Kalumuna na Diwani wa
Kata ya Nyanga Mh. Deusdedit Mtakyawa wote wa Chama cha Mapinduzi.
Tukio
lililo endelea ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya na
inasadikiwa kutokana na kura zilizopigwa nyingi ni zile zinazo
mshinikiza Mh. Amani kujiuzuru hivyo ndivyo mambo yalivyo.
Pia
kesi ya suala la soko kuu la Bukoba iko mahakamani kwani
wafanyabiashara wanapinga kubomolewa soko hilo kwani hakuna sehemu ya
kuhamishiwa kwa wakati wote wa ujenzi wa soko jipya
Post a Comment