Spika wa Bunge la Tanzania
Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na
kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati)
Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Makanu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo
ya Nje, Ulizi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb). Kulia ni Mhe. Sadifa Juma
Khamis, (Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kudhuria Mkutano wa
tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la Kibunge lanchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu.
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu
wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes
Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye
mkutano huo.
Spika Makinda na Spika wa
Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano
huo.
Picha ya pamoja ya maspika,
Sekretarieti pamoja washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR. Picha na Prosper
Minja-Bunge
Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika.
Pongeli hizi zimetolewa leo
na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye mkutano wa tatu
unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimewataja Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama
wapenda amani barania Afrika.
Hii ni kutokana na viongozi
hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya
Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya
uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nay
imepongezwa.
Bunge la Tanzania
limewkilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao
ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe. Pauline Gekul, na Mhe Sadifa Juma. Wengine ni
Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana Kikwembe.
Post a Comment