Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta
akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba katika mkutano baina yao katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi.
Maria Kashonda.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta
(katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt.
Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro Mohammed (kulia) mara baada
kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za
Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt.
Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano
kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba leo (jumatatu januari 21, 2013) jijini Dar es Salaam. Kushoto
kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju na Wajumbe
wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo
Kamishina wa Tume ya Kurekebisha
Sheria (LRCT) Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi maoni ya LRCT hiyo kuhusu
Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga
Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari
21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohammed.
Mjumbe wa Mtandao wa Kinga Jamii
(TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi. Clotilda Isdor akitoa
maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko uliofanyika leo (jumatatu janauari, 21, 2013). Wa kwanza
kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.
Post a Comment