AFYA
za wakazi na
wafanyabiashara wanaotegemea soko la wapiwapi wilayani Masasi mkoani
Mtwara zimo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu
kutokana na kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa taka ngumu katika eneo la soko hilo zilizo dumu kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Bahadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na mwananchi
jana kwenye eneo hilo la soko hilo walisema kuwa kutokana na hali hiyo ya
kuwepo kwa mlundikano wa takataka ngumu ambazo zimezagaa kandokando ya soko hilo
kunawafanya wafanyabiashara na
walaji kuwa katika hali ya hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko
ikiwemo kipindupindu jambo linalohatarisha afya
zao hasa kipindi hiki cha masika ambapo takataka hizo hunyeshewa mvua na
kusababisha kutoa harufu mbaya.
Walisema kuwa ili kuokoa hali ya kuwepo
kwa mlipuko wa magonjwa,wafanyabiashara hao wameiomba halmashauri ya mji Masasi
kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha takataka hizo zinaondolewa ili
kuyaweka mazingira ya soko hilo kuwa katika
hali ya usafi tofauti na yalivyo hivi sasa na kwamba hali hiyo pia inaweza kuwa
athiri hata wateja wanaokwenda kununua bidhaa katika soko hilo, hatua ya
utupaji wa takataka katika eneo hilo umewashangaza wafanyabiashara hao na baadhi
ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwa eneo hilo
sio maalumu kwa utupaji wa takataka.
Wakizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara
wenzao katika soko hilo,Siajabu Namadi,Hamisi Saidi walisema kuwa kwa sasa eneo
hilo limekuwa likitumika kwa utupaji takataka na baadhi ya vibarua wa
halmashauri ya mji pindi wanapozikusanya
kutoka katika maeneo mbalimbali wilayani humo ikiwemo kutoka stendi kuu ya
mabasi.
Walisema kuwa kuwepo kwa mlundikano huo wa takataka ambazo zimezagaa kando ya soko hilo kuna
hatarisha afya kwa wafanyabiashara wa soko hilo na wenda hali hiyo ikasababisha
kuibuka kwa magonjwa mbalimbali ya mlipuko iwapo halmashauri hiyo isipo chukuwa
hatua za makusudi kuziondoa takataka hizo.
Post a Comment