Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira (katikati), akipunga bendera wakati wa mkesha wa mwaka wa kuliombea Taifa uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Wasira alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkesha huo ulioshirikisha madhehebu ya Kikristo 50. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha huo Askofu Kenneth Damas kutoka Mighty Revival Ministries.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Madeye (kulia), Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Elizabeth Petro (kushoto), na Mbunge wa viti maalumu (CCM), Mbeya mjini Dk. Mary Mwanjelwa wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wananchi na waumini wa dini ya Kikristo wakishangilia baada ya kuvuka mwaka mpya.
Brasi Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani kwenye ibada ya mkesha huo wa mwaka mpya 2013.
Waimbaji wa kwaya mbalimbali wakitumbuiza. (PICHA HABARI NA WWW.MWAIBALE.BLOGSPOT.COM)
………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira amesema kuwa amani iliyopo Tanzania inatakiwa itumike kupambana na ufisadi.
Pia amesema amani ambayo ni haki ya kila mtu na Taifa la Tanzania inatakiwa itumiwe kudumisha haki kwani amani ni tunda la haki.
Wazira alitoa kauli hiyo katika mkesha wa kuukaribisha mwaka 2013 Dar es Salaam juzi ambao uliratibiwa na jumla ya makanisa 50 nchini.
Alisema si sahihi mtu kuilipia haki bali ni stahili ambayo mtu anatakiwa aipate bila kutozwa fedha ila wapo baadhi ya watu hukiuka hali halisi ya utoaji haki kwa kudai malipo.
Waziri Wasira alisema kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa kuhakikisha amani ambayo pacha wake ni maendeleo vinalindwa kama mboni ya jicho.
Mbali ya kuzungumzia suala la amani, Wasira alisema sheria nyingi za nchi zinazingatia kuwajali wananchi wake hasa inayohusu ardhi.
Alisema sheria nzuri ya ardhi inayotumika nchini imewawezesha wananchi kumiliki ardhi na kuifaidi hasa watu wanaoishi vijijini hulindwa na kupewa heshima kubwa kwa kumiliki ardhi tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine.
Wasira alisema zipo baadhi ya nchi ambazo hazina sheria inayowaruhusu watu kumiliki ardhi bali hubaki kuwa haki miliki ya Serikali.
Kutokana na sheria hiyo ya ardhi, Wasira alisema kulalamika na kulaumu havitaweza kuleta maendeleo ya watu na taifa lao isipokuwa kuzidisha uwajibikaji.
Alisema wapo watu ambao kazi kubwa waliyonayo ni kutafuta maneno matamu ya kulalamika na kulaumu badala ya kutumia muda huo kutafuta ufumbuzi wa mambo.
Mkesha huo uliozihusisha taasisi za dini ya Kikristo 50 ziliongozwa na Askofu Emmanuel Malasi ambaye katika maneno yake kubwa alilokuwa akisisitiza ni kudumisha, amani, upendo na uvumilivu.
Kwenye mkesha huo wa kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 walihudhiria viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dodluck Ole Medeye na Mbunge wa Viti Maalumu Mbeya, Dk. mary Mwanjelwa.
Pia zilikuwepo nafasi za uwakilishi katika idara na mashirika mbalimbali ya kimataifa huku ubalozi wa Marekani nao ukiwakilishwa na Elizabeth Petro.

Post a Comment