Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid
(mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa
kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea
Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan.
17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje
ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama
Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya
ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini
Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya
Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo
anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya ngoma mbalimbali
za utamaduni alipowasili katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha
Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya
Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Aliengozana nae
wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora
Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Kikundi
cha kinamama cha ngoma ya Msanja kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
salma Kikwete (hayupo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa
Kilimanjaro (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa
MAELEZO).
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma
Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)
wakati alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA)
Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John
Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan
16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi
linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama
atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto
ipewe kipaumbele.
Kauli hiyo imeendelea kutolewa na Mke wa Rais mama Salma
Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo
jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu
yatakayosaidia kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua.
Mama kikwete alisema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa
kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza maisha hapa nchini na
kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu walioupata kuchangia
kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua sanjari na watoto huku
wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati wakijifungua.
“Asilimia 90% ya nchi zilizoendelea wanaweza kupunguza ama
kuokoa maisha ya kinamama na watoto huku hapa nchini wakiandaa mpango
endelevu wa kuokoa maisha ya wamamawajawazito wakati wa kijifungua na
kutoa rai kuwa wamama wasife kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa
tiba”alisema mama Salma.
Mama Salma alisema kuwa suala la afya ya uzazi liwe mpango
endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na kuitaka serekali kulipa
kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha ya majukumu mbali mbali
iliyonayo.
Nae naibu waziri wa Afya na maendeleo ya jamii hapa nchini Seif
Raishid alisema kuwa serekali kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele
suala la mama afya ya uzazi na kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati
akiwa analeta kiumbe duniani sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza
wigo wa kuwafikia wakinamama kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na
usafiri sanjari na huduma muhimu.
Rashid akwataka watanzania walioshiriki kongamano hilo kutoa
uzoefu walioupata kutatua tatizo la afya ya mama na watoto ilikupunguza
vifo ambvyo vinawezekana kuepukika kutokana na kukosa eidha huduma
muhimu wakati wakujifungua.
Kwa upande wake mkurugenzi wa afya dkt dumilia chalamila
alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha zaidi ya wataalam na watoa
maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni wakichangia
uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la afya ya uzazi.
Post a Comment