Baada
 ya ziara kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo,pia Steve 
Gannon alipata wasaa wa kukaa meza moja na uongozi wa juu wa kampuni 
hiyo na kuzungumza machache,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ufanisi wa 
kikazi kwa mwaka mpya wa 2013. 
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto 
akichanganua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya 
Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa
 kabisa,iliyofungwa mjengoni humo,ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi
 karibuni,Steve Gannon amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na 
kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli 
mbalimbali zinavyofanyika mjengoni humo.
Steve
 Gannon akitazama picha za wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika 
nchini Tanzania na kufanya maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime 
Time Promotions Ltd.
Mkurugenzi
 wa mambo ya utafiti na vipindi vya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba 
akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya 
Serengeti,Steve Gannon ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.

Mkurungezi
 Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akimuuliza jambo 
mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Gerald Hando kuhusiana na 
mambo mbalimbali ya kikazi,alipotembezwa kwenye studio ya ziada.

 Mkurugenzi
 Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto 
akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya 
Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa 
wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna 
shughuli mbalimbali zikifanya mjengoni humo.

Mkurungezi
 Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akizungumza jambo 
na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.

Steve
 Gannon akisalimiana na Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions 
Ltd.Balozi Kindamba,mara alipotembelea ndani ya kampuni hiyo ambayo 
imekuwa ikijihusisha na matamasha mbalimbali likiwemo tamasha kubwa la 
Fiesta ambalo hufanyika kila mwaka.


Mkurungezi
 Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akioneshwa matoleo
 mbalimbali ya jariba la burudani la KITANGOMA linachapishwa na kampuni 
ya Prime Time Promotions.

Mkurungezi
 Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akipeana mkono na 
Mmoja wa wafanyakazi wa Prime Time Promotions,Godliva Nicholaus mara 
alipowasili ndani ya ofisi za kampuni hiyo.

Mkurugenzi
 wa mambo ya Masoko na Mauzo,Shebba Kusaga akifafanua jambo 
kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon.

Chief
 Editor wa Clouds TV,Bwa.Kanyopa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na 
ufanyaji wao kazi ikiwemo na urushaji wa vipi kupitia Tv yao,Pichani 
kushoto ni Boss Joe akisikiliza kwa makini.

Mkurungezi
 Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon alitembezwa pia 
ndani ya chumba maalum cha kuandalia habari,hapa Mtangazaji wa kipindi 
cha Michezo Shaffih Dauda akifafanua jambo kwa Steve Gannon.Picha Hizi Zimeletwa hapa na JIACHIE BLOG.


Post a Comment