Wanafunzi wa 
Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele 
ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na
 nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi 
kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na 
majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya 
kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku 
waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili 
wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. 
Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama 
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti. 
 | 
Ulinzi uliimarishwa nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi. 
 | 
Kamanda wa 
Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman 
Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara 
baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo 
aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo 
walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova 
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita. 
 | 
"Wanafunzi wenzetu wa kiume 
wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatuna ulinzi 
tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo" 
 | 
Baadhi ya 
wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye 
kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda 
Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova. 
 | 
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni. 
 | 
Kova akitoa maelezo kwa waandishi 
wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo 
ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni 
kufuatilia tukio hilo kwa pamoja. 
 | 
Mitaani Posta. 
 | 
Hadi kieleweke! 
 | 
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni. 
 | 
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli. 
 | 
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure! 
 | 
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue! 
 | 
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria 
 | 
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa 
wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote 
na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya 
tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na 
ikielekea Kigamboni.Picha Kwa Hisani Ya Mtaa Kwa Mtaa Blog 
 | 



Post a Comment