Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzbar Msham Abdulla Khamis akifungua mkutano wa
tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 kwa
niaba ya Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na
Watoto Bi. Zainab Omar Mohammed leo mjini Zanzibar.Mkutano huo
umewashirikisha viongozi na waratibu wa mbio za mwenge kutoka maeneo
mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.
Mwenyekiti
wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 ambaye pia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.
Sihaba Nkinga (kulia) akiongoza mkutano huo leo mjini Zanzibar. Kushoto
ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Lufunga mkoa ambao ulikua mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2012.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge mwaka 2012
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano
huo kuhusu , mafanikio, changamoto na namna ya kufanikisha shughuli za
mbio za Mwenge nchini.
Mratibu
wa Mbio za Mwenge mkoa wa Iringa Bw. Atilio Mganwa akitoa mchango wake
kuhusu uboreshaji wa shughuli za mbio za Mwenge nchini ambapo mkoa wa
Iringa utakuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa Mwaka 2013.
Washiriki
wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kutoka maeneo
mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea mjini Zanzbar.
Post a Comment