Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati) akikagua gwaride la heshima la
wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa
matreka kozi namba 7 katika Chuo cha Udereva na Ufundi cha jeshi hilo (KPF)
kilichopo Kingolwira nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimpongeza Beatrice Dugange baada ya kumpa
cheti na leseni ya udereva baada ya kumaliza mafunzo ya udereva chuoni hapo.
Jumla ya wanafunzi 66 walipatiwa vyeti na leseni kwa kuhitimu mafunzo hayo.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna
Jenerali John Minja akitoa hotuba yake na baadaye kufunga mafunzo hayo ya
awali.
Wanafunzi wa Shule ya
Msingi Mkono wa Mara iliyopo chuoni hapo wakitumbuiza katika sherehe hiyo kwa
kutoa michezo mbalimbali mbele ya mgeni rasmi, Kamishna Jenerali John
Minja.
Baadhi ya wahitimu
wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja wakati akitoa hotuba yake na baadaye kuyafunga mafunzo ya udereva wa
magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI
Post a Comment