Mwanamitindo maarufu duniani Naomi Campbell amepata majeraha ya ndani katika mguu wake wa kushoto baada ya kuvamiwa na kuibiwa na majambazi katika mitaa ya Paris.
Mwanamitindo huyo nyota duniani ameonekana siku za hivi karibuni akifunga usaidizi katika mguu wake na sasa imewekwa wazi kuwa alishambuliwa na kundi la wahuni wakati alipokuwa akijaribu kukodi taxi katika mji mkuu wa Ufaransa.
Mpaka sasa haijulikani walimuibia vitu vyenye thamani ya shilingi ngapi, lakini inaaminika kwamba wahuni hao walilenga kupora vito vya thamani.
Naomi Campbell akiwa kwenye Wheelchair baada ya kujeruhi mguu wake wa kushoto ba vibaya.
Mchumba wa Mwanamitindo huyo Vladimir Doronin (42) amemsafirisha Naomi kwa kutumia ndege binafsi hadi Vail, Colorado ambako ametibiwa na Richard Steadman ambaye ni mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji wa mifupa duniani.
Naomi amekuwa akitumia kiti cha magurudumu na magongo ya kutembelea kufuatia shambulio hilo na mchumba wake Vladmir ameimarisha ulinzi popote mrembo huyo anapokuwepo.



Post a Comment