
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana,
amewataka viongozi wa dini nchini kuendesha shughuli za
imani
wanazoziamini kwa kuheshimiana.
Mbali
na kutaka waheshimiane
alitaka wote wasiopenda
kubaguliwa
dini na imani zao
wasiwe wepesi wa kukashifu imani
na
dini za watu wengine.
Hayo aliyasema wakati wa maadhimisho ya siku ya
Imam Hussein, yaliyofanywa na Dhehebu la Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat
Arusha.
Maadhimisho hayo hufanyika duniani kote ambapo
mkoani Arusha yalifanyika kwenye Msikiti wa Jumuiya hiyo na kuhudhuriwa na
viongozi wa madhehemu na viongozi wa chama na serikali.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Kinana
alisema, changamoto zinajitokeza sasa za baadhi ya watu kukashifu dini nyingine
zinapaswa kukemewa na kupingwa.
Alisema pamoja na yote kujitokeza bado Serikali
inaendelea kuwa makini na kuwa macho kwa kuhakikisha inawadhibiti watu wenye nia
ya kuangamiza amani ya taifa.
“Dini zote nchini zinapaswa kuendesha shughuli
zao kwa kuheshimiana. Msingi ya taifa letu inatutaka tusidharau imani wala
itikadi ya mtu mwingine.
“Kama wewe haupendi kubaguliwa kwa dini au
imani yako, basi usiwe mwepesi wa kubagua imani au dini ya mtu mwingine,’’
alisema Kinana.
Katibu Mkuu huyo wa CCM, aliwaeleza viongozi
hao kwamba kwa muda mrefu sasa amekuwa akikerwa na chokochoko hizo ambazo zina
kila dalili ya kuondoa amani iliyopo.
“Nitoe wito kwa Taasisi za dini nchini
ziendelee kuhubiri amani kwa kuliombea taifa, ili Watanzania waendelee kujivunia
amani iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema
Kinana.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli,
Jowika Kasunga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema Serikali
ipo macho katika kuhakikisha amani inaendelea kulindwa.
Alisema mbali na kuendelea kulinda amani
iliyopo Serikali inatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini nchini katika
kuboresha na huduma za kijamii kwa wananchi.
“Niwaombe viongozi wa dini nchini muendelee
kudumisha amani iliyopo, kwani tukiendelea kuona baadhi ya wachache wakiichezea
gharama ya kuirudisha ni kubwa.
“Tumepata taarifa za baadhi ya watu kujipenyeza
ili wavuruge amani kwa kutumia mgongo wa dini, sisi tumejipanga kuhakikisha kila
mwananchi anaishi kwa uhuru wa kuabudu mahali popote,” alisema
Kasunga.
Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Khoja Shia,
Gulam Hussen, alibainisha kwamba maadhimisho hayo yanalenda kukumbuka mazuri
aliyoyafanya Mtume Mohamad.
“Maadhimisho haya yanatambulika kwa jina la
‘Hussein Day’ yanajenga undugu kufahamiana na kupinga ufisadi unaolinyemelea
taifa kwa baadhi ya viongozi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali,” alisema
Hussein.


Post a Comment