Na Elizabeth John
RAIS wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi anatarajia
kuwa msimamizi Mkuu katika pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la
Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Ngowi anatarajiwa kuwa
msimamizi Mkuu katika mpambano huo utakaowakutanisha mabondia Ilunga Makaba
kutoka Jamhuri ya Kidokrasia ya Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya
Kusini na Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia.
Ngowi alisema, pambano la
wawili hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana
kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la
Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight Februari 15 mwaka huu
katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji
la Johannesburg.
Ngowi kama kamishena mkuu wa
pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao ambapo mwamuzi ni Wally Snowball,
Jaji namba moja Simon Xamlashe na namba tatu Jaap Van Niewenhuizen wote kutoka
(Afrika Kusini) pamoja na Jaji namba mbili Manuel Maritxalar
(Spain).
Aliongeza kuwa pambano hilo
ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini
ya uradi wa IBF
Post a Comment