KWA
UFUPI:
Akisimulia
tukio hilo, mkazi wa kitongoji hicho, aliyejitambulisha kwa jina la Yusuph Kondo
(80) alisema mchana wa jana alimwona Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa akiwa na
kidumu cha mafuta na kwamba alielekea kwenye nyumba ya Zaituni Mguguli na mara
baada ya kufika eneo hilo aliona moto ukiunguza nyumba.
NYUMBA 19
ambazo idadi ya wakazi wake haikujulikana mara moja zimeteketea kwa moto
unaodaiwa kuwashwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa akishirikiana na polisi wa
Kituo ch Staki Shari jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo
zilijengwa katika Mtaa wa Vikongoro, Kata ya Chanika Wilaya ya Ilala katika
eneo ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro.
Akisimulia
tukio hilo, mkazi wa kitongoji hicho, aliyejitambulisha kwa jina la Yusuph Kondo
(80) alisema mchana wa jana alimwona Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa akiwa na
kidumu cha mafuta na kwamba alielekea kwenye nyumba ya Zaituni Mguguli na mara
baada ya kufika eneo hilo aliona moto ukiunguza nyumba.
Naye mtoto
wa Zaituni aitwaye Ajuaye Twaha(10), alisema walifika mwenyekiti akiwa na askari
na kumwamuru atoke nje na kwamba alimuona askari akimwagia mafuta na kuwasha
moto.
Miongoni
mwa wakazi waliopata hasara kutokana na tukio la kuungua nyumba zao, ni Fikiri
Hassan, Zuberi Kiiba, Asha Abdallah, na Issa Salehe.
Ofisa
Mtendaji wa mtaa huo, Ali Kambi, alipoulizwa juu ya tukio hilo alikiri na
kwamba lilitokana na mgogoro wa ardhi.
Alisema
waliochomewa nyumba wote walivamia eneo la mtu anayeitwa Nicolaus Malose
aliyemilikishwa na kijiji tangu 2011.
Hata hivyo waathirika wa tukio hilo walisema eneo hilo ni lao tangu mwaka 1985.
Hata hivyo waathirika wa tukio hilo walisema eneo hilo ni lao tangu mwaka 1985.
Mkuu wa
Kanda ya Kipolisi Ilala, Marietha Minongi Komba alipoulizwa jana kuhusu tukio
hilo alisema hakuwa na taarifa za kuungua kwa nyumba na kwamba siku ya jana
alizungumza na Mkuu wa Kituo cha Polisi Ukonga mara saba, lakini hakupata
taarifa zozote
Post a Comment