baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa jeshi la polisi mkoa wa iringa na mkuu wa mkoa
MKUU wa
Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma amezindua mradi wa Mkaguzi wa
Tarafa wa Polisi Mkoa wa Iringa na kutaka jeshi hilo kushirikiana na
wananchi katika utendaji kazi ili kufanikisha malengo yake ya kuweka mji
katika hali ya amani na utulivu na kuepukana na matumizi ya nguvu na
kuwa jirani zaidi na jamii kwa lengo la kupata taarifa zaidi za ulinzi
shirikishi na kuwajua waharifu.
Alisema
hayo wakati akizindua mradi huo ulionza kuzinduliwa rasmi kitaifa tarehe
11 mwezi wa 1 mwaka huu na Inspekta Jenarali wa Polisi Said Mwema jiji
Dar es Salaam na polisi kushirikiana na wananchi katika ulinzi
shirikishi kwa lengo la kuleta amani na kupunguza uhalifu katika jamii.
“Kwa kuwa
wananchi wanajua matukio mengi pamoja na waharifu hamna budi
kuwashirikisha na kuwa nao jirani kuweza kufanya nao kazi kuweza kuleta
taarifa sahihi kwenu hivyo muwe nao jirani” alisema Ishengoma.
Aidha
aliwapongeza jeshi la polisi mkoani hapa kwa kuweza kupunguza kwa kiasi
kikubwa makosa makubwa ya uhalifu hadi kufikia asilimia 4.4 kwa kipindi
cha mwaka 2012 na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwa mwaka huu na
kumaliza kabisa makosa hayo kwa kuwatumia wakaguzi wa tarafa.
Dk
Christine Ishengoma katika uzinduzi huo alikabidhi pikipiki 18 kwa
maafisa wa polisi ambao ni wakaguzi wa tarafa 15 huku pikipiki tatu
zikikabidhiwa kwa kikosi cha usalama barabarani aliwataka polisi mkoani
hapa kuepuka kujihusha na vitendo vya uharifu akidai kufanya hivyo
kunaathiri utendaji kazi kwa jeshi hilo kama baadhi ya mikoa iliyokutwa
na polisi wakijihusisha na makosa ya kinidhamu na kuwasisitiza kuzitumia
kwa uangalifu pikipiki hizo ziweze kudumu.
Awali
akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa
Kamshina msaidizi wa Jeshi la Polisi Kamanda Michael Kamuhanda mkoani
alisema kwamba lengo la mradi huo ni kupunguza uharifu kuanzia ngazi ya
familia,mtaa, kitongoji, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi ngazi ya
kitaifa ili kuimarisha maendeleo ya ustawi wa jamii.
Aidha
Kamanda Kamuhanda aliongeza kwamba lengo la mpango huo ni kuunganisha
kila familia katika kutambua viashiria vya uvunjifu wa amani, stadi za
utatuzi wa migogoro na umuhumu wa ustawi wa jamii katika mkoa wa Iringa.
“Ieleweke kwamba wamiliki halisi wa mradi huu ni wakaguzi wa tarafa na
sio vinginevyo” alisema
Kamuhanda
aliwataka wakaguzi wa tarafa wayatambue maeneo yao ya kazi, kuwatambua
wakazi wa maeneo hayo aidha kuwatambua wadau wa polisi jamii na
kushirikiana nao kwa kuandaa mpango kazi kwa kutoa elimu kwa jamii hiyo.
“Wakaguzi
wa tarafa watahakikisha wanaratibu na kusimamia miradi yote ya polisi
na jamii kwa kushirikiana na vitengo vingine na vikosi vyote katika
maeneo yao kama madawati ya ukatili wa kijinsia, intelejensia, kampuni
binafsi za ulinzi” alisema Kamuhanda“
Mkuu huyo
wa jeshi la polisi mkoani hapa alitaja Kauli mbiu ya jeshi la hilo ni”
Doria na misako kwanza,ushirikishwaji wananchi kwanza kazi za ofisini”
Post a Comment