*****************
WAZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, amepinga vikali hatua ya wabunge kujiongezea marupurupu ya kustaafu na kuitaja kama uhalifu na ulafi mkubwa ambao unapaswa kupingwa na Wakenya wote.
Odinga alitoa msimamo huo muda mfupi baada ya taarifa kwamba wabunge walipitisha kwa siri mpango wa kujipatia kiinua mgongo cha Sh9.3 milioni (Sh150 milioni za Tanzania) kila mmoja.
Iwapo muswada huo utapitishwa, marupurupu ya wabunge wote yatagharimu Sh2.6 bilioni za walipakodi wa Kenya (Sh46.8 bilioni za Tanzania).
Iwapo muswada huo utapitishwa, marupurupu ya wabunge wote yatagharimu Sh2.6 bilioni za walipakodi wa Kenya (Sh46.8 bilioni za Tanzania).
Alisema kwamba hatua hiyo haikubaliki na inamaanisha kuyapaka matope mafanikio ya Bunge la 10 na Serikali ya Muungano inayomaliza muda wake Machi mwaka huu.
Odinga alisema kuwa hatua hiyo ya Wabunge ya kupitisha miswada ya kuongeza marupurupu ya Rais, makamu wa Rais na maofisa wengine wakuu wa Serikali inalenga kumhonga rais akubali ulafi wao wa kujipatia mabilioni ya pesa kama kiinua mgongo watakapostaafu.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari juzi, Odinga aliitaja hatua hiyo ya Jumatano usiku kama isiyokubalika na kwamba anashauriana na rais ili kuhakikisha kuwa marupurupu hayo hayapitishwi.
“Kupitishwa kwa miswada hii ni ujanja wa Wabunge na hatua ya kumshinikiza na kumhonga rais akubali mahitaji yao. Hii ni tamaa ya hali ya juu ambayo inastahili kukashifiwa na kupingwa na Wakenya wote. Ninapinga marupurupu hayo ambayo hatuwezi kuyamudu,” alisema Odinga.
Waziri Mkuu alisema kuwa marupurupu hayo hayafai kwani Wakenya wengi bado wanateseka kutokana na majanga ya njaa, ukosefu wa usalama, ukosefu wa ajira, afya duni na garama ya juu ya maisha.
Waziri Mkuu alisema kuwa marupurupu hayo hayafai kwani Wakenya wengi bado wanateseka kutokana na majanga ya njaa, ukosefu wa usalama, ukosefu wa ajira, afya duni na garama ya juu ya maisha.
“Ninashauriana na rais kuhusu suala hili ili kuhakikisha kuwa tunafanya uamuzi ufaao kwa watu wa Kenya,” alisema Odinga. Iwapo sheria hiyo itawekwa sahihi na rais, kila mbunge atapewa mlinzi mwenye silaha, mazishi ya kitaifa na paspoti ya kibalozi pamoja na mkewe au mumewe.
Wabunge pia wataruhusiwa kutumia eneo la watu mashuhuri (VIP) katika viwanja vya ndege kote nchini.
Wabunge pia wataruhusiwa kutumia eneo la watu mashuhuri (VIP) katika viwanja vya ndege kote nchini.
Hii ni mara ya pili kwa wabunge kupendekeza suala la kulipwa mabilioni ya pesa baada ya kipindi chao kukamilika.
Hali hiyo ilikuja baada ya Waziri wa Fedha, Njeru Githae kufanya kikao siku ya Jumatano usiku na kushirikiana na wabunge hao kupitisha sheria itakayoruhusu malipo ya fedha hizo baada ya kipindi cha Bunge la 10 kukamilika.
Katika kikao hicho, waliazimia kuwa mawaziri wote 42 katika Serikali ya sasa ya muungano na manaibu wao 55 kupewa dereva atakayelipwa na Serikali na kunufaika na marupurupu yote ambayo Bunge litapitisha.
Hali hiyo inadaiwa kuwa ni njama ambayo imeundwa kwa ajili ya kuilaghai Serikali pamoja na kujilimbikizia mali.
Walipitisha kwamba baada ya kipindi chao kukamilika, walipwe asilimia 31 ya mshahara wao wa kila mwezi ambao walihudumia Serikali.
chanzo: Mwananchi
chanzo: Mwananchi
Post a Comment