Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Inspekta Jenerali wa
Polisi katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumlaki
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
Kamishna Robert Manumba aliyelazwa hospitalini hapo-
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa
Jeshi la Polisi (DCI), Robert Manumba bado ni tete na jana Rais Jakaya Kikwete
alikwenda tena ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika Hospitali ya Aga Khan, Dar
es Salaam alikolazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), kumjulia
hali.
Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine waliofika hospitalini hapo kumjulia hali DCI Manumba ni Mke wa Rais, Salma, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Said Mwema na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni. Pia walikuwapo ndugu, jamaa na marafiki ambao walikusanyika hospitalini hapo takriban siku nzima jana wakifuatilia afya yake.
Rais Kikwete alifika hospitalini hapo jana saa 11:15 na alitumia takriban dakika 10 tu kwani alitoka saa 11:26 huku akionekana mnyonge na alielekea kwenye gari lake na kuagana na IGP Mwema na Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee kisha kuondoka.
Post a Comment