Rais Barack Obama akiapishwa na Jaji Mkuu wa Marekani, John Roberts kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili Ikulu ya White House jana. Kulia ni watoto wake, Malia na Sasha. Picha na AFP.
Rais Barack Obama
aapishwa rasmi kwa muhula wa pili na Jaji mkuu John Roberts katika White House,
Januari 20, 2013.
Rais Barack Obama, wa
Marekani alipomshinda mgombea kiti wa chama cha Republican Mitt Romney, ili
kuingia madarakani kwa mhula wa pili akiwa na familia yake.
Obama ambaye
ni Rais wa 44 wa Marekani, aliingia madarakani katika uchaguzi wa kihistoria
mwaka 2008 uliomfanya kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika taifa
hilo kubwa duniani.
Sherehe za
kuapishwa kwake Ikulu jana zilikuwa za faragha na zilihudhuriwa na watu wachache
maalumu, leo ataapishwa katika sherehe za jumla zitakazowajumuisha watu wote
kwenye Uwanja wa National Mall.
Katika kiapo
chake, Obama atatumia Biblia mbili, moja iliyokuwa ikitumiwa na Martin Luther
King na nyingine ilikuwa ikitumiwa na aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham
Lincoln.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Martin Luther
King ambaye alikuwa mchungaji na mwanaharakati wa haki za watu wenye asili ya
Afrika nchini Marekani, aliuawa Aprili 4, 1968, muda mfupi baada ya kutoa hotuba
yenye nguvu ya I have a Dream (Nimeota ndoto).
Hotuba hiyo
ikuwa ikieleza ndoto yake kwamba muda siyo mrefu watu wenye asili ya Afrika
watapata nguvu na kupata haki yao kama raia wa Marekani.
Viongozi hao
wawili wana historia ya pekee, Lincoln ndiye aliyetumia muda wake mwingi akiwa
Ikulu ya Marekani kuhakikisha watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa watumwa
wananasuliwa utumwani.
Luther
alikuwa mwanaharakati aliyechochea mabadiliko kwa kushinikiza Serikali kuwapa
haki zao za msingi.
Obama
aliapishwa rasmi jana ikiwa ni siku ya kwanza kati ya siku mbili zilizopangwa,
leo ataapishwa mara ya pili katika viwanja maalumu vya Nationa Mall mjini
Washington, ambako maelfu ya watu watapata fursa ya
kushuhudia.
Hotuba ya
kuapishwa kwake itakayotolewa leo inatarajiwa kuweka historia mpya, pia
kuhitimisha matukio ya siku mbili hizi za kuapishwa, ataweka wazi mtazamo wake
wa kipindi cha miaka minne ijayo.
Mkusanyiko
utakaoshuhudia kuapishwa kwake na kusikiliza hotuba yake moja kwa moja katika
uwanja huo unakadiriwa kupungua kutoka ule wa watu 1.8 milioni mwaka 2009 na
kufikia kati ya 600,000 na 800,000, huku mamilioni wakishuhudia kupitia
televisheni.
Post a Comment