* NI MARUFUKU WALIMU KUWAREJESHA WANAFUNZI NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA ADA
Serikali
imepiga marufuku Wakuu wa shule za Sekondari wote nchini kuwarudisha
nyumbani wanafunzi kwa kisingizio cha kukosa Ada na michango ya aina
yeyote ya aina mbalimbaliwatoto wanaoshindwa kuchangia na kulipa Ada
kutokana na ama wazazi kutokawa na uwezo wa kulipia kwa wakati michango
hiyo.
Agizo
hilo limetolwa jana na Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri wakati wa
ziara yake mkoani katavi mara baada ya kutembelea shule ya sekondari ya
Nsimbo Mkoani Katavi na kusomewa taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi
wanashinwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa ada na michango
mbalimbali inayotolewa mashuleni kutokana na wazazi waokuokuwa na uwezo.
“Ni
marufuku kwa mkuu yeyote wa shule kuwrudisha nyumbani watoto kwa sababu
ya kukosa ada ikiwamo michango ya madawati kwani kumrudisha nyumbani
mtoto ni kumuonea michango hiyo adaiwe mzazi wakati mwanafunzi
akiendelea na masomo”alisema Naibu waziri.
Alieleza
kuwa michango yote inayotakiwa kukubaliwa shule ni lazima Katibu
Tawala wa mkoa husika aione na kuridhia kwenye barua na siyo wakuu wa
shule kujiamulia kienyeji hali inayoonesha kuwarudisha nyumbani wato
ambao hawana Michango hiyo ikiwemo ya madawati.
“Hivi
hiyo michango ya madawati kila mwaka madawati hayo yanaenda wapi kwa
kuwa kila mwaka mtoto anapoanza kidato cha kwa anaambiwa aende na
madawati sasa yanakwenda wapi kama siyo uzembe wa wahusika
yanapoharibika kuyatengeneza na kuyatunzo madawati hayo
yapoharibika”alisema.Mwanri.
Katika
hatua nyingine akizungumzia suala la madarasa manne ya shule ya
sekondari ya Kashaulili iliyoko Halmashauri ya Mji wa Mpanda kujengwa
chini ya kiwango na shilingi milioni nane zilizotolewa kwenye akauti
bila utaratibukufuatwa ambazo zilikuwa za ujenzi wa shule hiyo
zifuatiliwe.
Kutokana
na kujengwa madarasa hayo chini ya kiwango amemwagiza Katibu Tawala wa
Mkoa wa Katavi Emmanuel Kalobelo kwa kusaidia na na Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima kufuatilia na kuona fedha zilitolewaje benki na
matumizi yake yakoje na wahusika ni watu gani kisha ikidhibitika kwamba
walitoa fedha Benki bila utaratibu unaoeleweka wahusika wachukuliwe
hatua za kisheria.
“Sasa
naagiza kuwa iwapo watabainika na kuonekana kweli makosa yalifanyika
wahusika wachukuliwe hatua za kisheria”alisema Mwanri kwa sauti ya
ukali.
Naibu
waziri alilazimika kutoa kauli hiyo kufuatiwa maelezo yaliyotolewa na
mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi wilaya ya Mpanda Hasani Segela
aliyetaka kufahamu hatima ya madarasa hatima ya madarasa hayo manne ya
shule hiyo ya sekondari ya kashaulili ambayo ni ya nguvu za wananchi
nkwa kuwa ni shule ya kata na watoto wanasomea hapo katika madarasa hayo
abayo yanweza kuleta madhara iwapo lolote likitokea.
Post a Comment