Vurugu
zimetokeaJana asubuhi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Mwanza mara
baada ya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuandamana na
kuwafanyia vurugu askari wa usalama barabarani ambao walikuwa katika
zoezi la ukaguzi wa pikipiki zinazofanya safari ndani ya jiji hilo.
Jeshi la
polisi lililazimika kuvurumisha risasi za moto hewani pamoja na mabomu
ya machozi ili kuwatawanya waendesha pikipiki hao waliokuwawakifanya
vurugu wakikusanyika toka sehemu mbalimbali za jiji kulazimisha wakaguzi
hao kuwaachia wenzao waliokamatwa kutokana na kuvunja sheria mbalimbali
za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na wengine kukosa leseni na
kukosa kofia mbili za usalama kwa mwendeshaji na abiria kama
ilivyoagizwa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mwanza, Everist Mangu anathibitisha kutokea kwa vurugu hizo.
|
Ilikuwa saka nikusake baina ya madereva wabishi wa pikipiki na askari wa jeshila polisi mkoa wa Mwanza. |
|
Gari la dolia likipita eneo la Mission kirumba jijini Mwanza kuhakiki hali ya usalama. |
|
Askari
wajeshi la polisi katika harakati ya kutawanya waandamanaji kwa njia ya
mabomuya machozi eneo la Mission Makongoro Kirumba jijini Mwanza. |
|
Hizi ni harakati za jeshi la polisi Mwanza kupakia pikipiki zilizonaswakwenye doria. |
|
Wanausalama barabarani kazini katika kuzibaini pikipiki zinazokiukataratibu na sheria za usalama barabarani. |
|
Mmoja
kati ya vijana walionaswa na jeshi la polisi kukiuka sheria na taratibu
za usalama barabarani akiwa kwenye difenda ya polisi naye akiomba
usaidizi kupitia simu yake ya mkononi kwa ndugu na jamaa haikufahamika
maramoja kwambaaliachiwa au laa kwani kwa wale waliokutwa na makosa
wengi walitozwa faini na kisha kuendelea na kazi , lakini kwa wale
waliosababisha vurugu rungu la sheria lawangoja. |
|
Wana usalama kazini. |
|
Machafuko. |
Post a Comment