* YANGA YAIBUTUA TENA BLACK LEOPARD 2-1 MWANZA
Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa timu ya Yanga wakifuatilia kwa makini mtanange uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo.Kwa picha zaidi Bofya JIACHIE BLOG.
Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 1 Black Leopard Magoli ya yanga yalifungwa na Bahanuzi dkk 3, Tegete dkk 53 kwa njia ya penalti huku goli la Black Leopard likifungwa na Obaje dkk 12
Huo ni ushindi wa pili kwa Yanga dhidi ya timu hiyo, baada ya awali kuwalaza 3-2 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga inarejea Dar es Salaam kesho, tayari kwa mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili dhidi ya Prisons ya Mbeya, Jumapili Uwanja wa Taifa. Leopard pia wanarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba kesho, Uwanja wa Taifa.
1.All Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Nurdin Bakari
7.Saimon Msuva
8.Kabange Twite
9.Said Bahanuzi
10.Hamis Kiiza
11.David Luhende
Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.Stephano Mwasika
4.Juma Abdul
5.Ladislasu Mbogo
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Omega Seme
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Jerson Tegete
11.Haruna Niyonzima
12.Yusuph Abdul
13.Rehani Kibingu
14.George Banda
15.Nizar Khalfani
16.Godfrey Taita
Post a Comment