Na: Gladness Mushi Arusha
SERIKALI
kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutekeleza mpango wa miradi ya
miaka mitano wa kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga wakati wa
kujifungua na walio chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuboresha
huduma ya mama na mtoto na kuokoa maisha yao.
Hayo
yameelezwa na Daktari bingwa wa akina mama na watoto wizara ya Afya na
Ustawi wa jamii ,Dk Koheleth Winani, kwenye kikao cha pamoja na baadhi
ya wakuu wa mashirika mbalimbali wanaohudhuria mkutano mkuu wa
kimataifa wa afya ya mama na mtoto, wanaoshirikiana na serikali
kutekeleza mpango huo wa kupunguza vifo vya mama na watoto nchini
walipokuwa wakitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali kwa wanahabari.
Dakta
Winani, amesema 75% ya watanzania wanaishi vijini ambako hawapati
huduma zilizo bora wakati wa kujifungua kutokana na umbali na maeneo
mengine kutopitika hasa wakati wa maska kutokana na miundo mbinu duni na
kusababisha wajawazito kujifungulia majumbani au wengine kupoteza
maisha wakati wakipelekwa kwenye Hospital , Vituo vya afya na Zahanati..
Amesema
kuwa mpango huo unalenga kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na
watoto 500 mwaka 2000 hadi kufikia 19 ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni sehemu
ya utekelezaji wa malengo ya Milenium, na kusisitiza kuwa ushirikiano
kati ya serikali na wadau hao ni muhimu kwa kuwa serikali peke yake
haiwezi kutekeleza mpango huo kwa ufanisi.
Kwa
upande wake daktari Dustan Bishanga, ambae ni mkurugenzi wa mradi wa
Maisha unaofadhiliwa na ,shirika la misaada la Kimarekani, USAID , kwa
kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2008 kwa thamani ya Dola milioni
40 umeboresha huduma ya afya ya mama na mtoto mchanga.
Dakta
Bishanga, amesema mradi umetengeneza mwongozo unaotumika na wadau
wengine kutekeleza mradi hiyo ,pia mradi huo unatengeneza mitaala ya
kufundishia watoa huduma kwa kushirikiana na wizara ya afya ili kutoa
mafunzo na uratibu wake katika vituo tofauti tofauti vipatavyo 250
nchini kote Tanzania bara na Zanzibar lengo ni kuboresha huduma ya mama
na mtoto mchanga na kuokoa maisha
Post a Comment