SHIRIKA
la Jhpiego la jijini Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya
mradi ujulikao kama Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za
mkononi kwa ajili ya kufuatilia afya za mama wajawazito kwa malengo ya
kupunguza vifo vya wajawazito
Meneja mradi wa shirika hilo
Dkt Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza
kutekelezwa kwa mkoa wa Morogoro
Dkt
Bishanga aliongeza kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa
inapunguza vifo vya mama wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya
kuwakutanisha wahudumu wa afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali
Pia
alisema kuwa Mradi huo ambao kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa
Morogoro lakini wanaendelea kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha
kuwa unasambaa nchi nzima kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha
ya mama wajawazito
Hataivyo
aliongeza kuwa mara baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo
wataweza kwenda mikoani ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi
ili kuimarisha zaidi afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo
hivyo vinasababisha sana Umaskini katika jamii.
Awali
alisema kuwa suala la mama wajawazito ni suala ambalo linatakiwa
kuchukuliwa tahadhari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu
sahihi za afya kutoka kwa wataalamu hivyo nao wazazi wa kiume wana
nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo
Post a Comment