Tanzania imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani ambapomfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha za umma
Hayo
yamebinishwa leo na mkaguzi mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed
Mtonga wakati akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika
kanda ya kaskazini
Mohamed
alisema kuwa mpango huo wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza
kutumika rasmi hapa nchini July Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha
viashiria mbalimbali ambavyo vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya
Serikali kuu pamoja na Serikali za Mitaa.
Alisema
kuwa kupitia mfumo huo mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza
kuboresha na kuwafanya wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru
zaidi tofauti na mfumo uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa
wakaguzi wa ndani
Alifafanua
kuwa hapo awali wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza
majukumu yao kutokana na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa
na uhusiano baina ya mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha
kukwamisha malengo mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje ndani ya
mfumo wa ukaguzi kimataifa suala hilo halipo kabisa.
“leo
tumewakutanisha wakaguzi wa ndani kutoka kanda hii ya kaskazini lengo
likiwa ni kuhakikisha kuwa wanabadilika na wanaanza kwenda na mfumo huu
mpya wa ukaguzi wa Kimataifa ili tuweze kufikia katika malengo
mbalimbali ambayo kwa kweli tunayataka sasa ni wajibu wa kila mkaguzi
wa ndani kuhakikisha kuwa anafuata kanuni hizi za Kimataifa na kama
hatafuata basi Sheria itambana”alisema Bw Mohamed
Katika
hatua nyingine alisema kuwa wakaguzi wa ndani bado wanakabiliwa na
changamoto ya uhaba wa bajeti hali ambayo nayo inafanya washindwe
kufanya kazi na kukagua miradi kwa wakati husika
Alisema
kuwa kwa sasa wakaguzi wa ndani wanashindwa kufika kwenye miradi tena
kwa wakati kutokana na uhaba wa bajeti ambazo zinatengwa na Halmashauri
huku hali hiyo pia ikichangia sana kutofikia malengo mbalimbali ya
kiukaguzi ambayo yanatakiwa kuwekwa na pia kusaidia jamii
Post a Comment