Umoja
wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya
kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika
baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililotolewa na
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa
maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa
hilo kwa miaka kadhaa.
Mwenyekiti
wa Umoja huo wa afrika ambaye pia ni rais wa Benin Boni Yayi ametoa
pongezi hizo jijini Dar es salama wakati alipokutana na mwenyeji wake
Rais Jakaya Kikwete kujadilia pamoja na mambo mengine migogoro
inayoendelea kulikumba bara la afrika na namna ya kusaka ufumbuzi wake.
Kiongozi
huyo wa madagasca ametangaza kwamba hatawania kwenye kinyang’anyiro
hicho ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwa na majadiliano na viongozi
wa sadc waliokutana jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusaka suluhu
kuhusiana na mzozo wa madaraka uliolikumba taifa hilo tangu mwaka 2009.
Kwa
upande wake Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyoongoza majadiliano ya
kupatikana suluhu ya kudumu, amesema kuwa nchi za sadc zimepokea
taarifa hiyo kwa furaha kubwa, na akaahidi uungwaji mkono kwa wananchi
wa madagasca.
Pamoja
na kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Andry Rajolina, kwa upande
mwingine Mwenyekiti wa Umoja huo wa Afrika umetoa wito kwa jumuiya ya
kimataifa kuunga mkono juhudi za kuwafurusha wanamgambo walioliteka eneo
la Kaskazini mwa Mali.
Post a Comment