|
KAMANDA DIWANI RPC MBEYA
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI KUACHA NJIA
KUGONGA NYUMBA NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 22/01/2013 MAJIRA YA SAA 18:30 HRS HUKO MAENEO
YA IMEZU KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA
MBEYA.. GARI NO T 905 AGX / T 844 ASK AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA ANUANI YAKE LILIACHA NJIA NA KUGONGA NYUMBA YA NDELE S/O
KWIMBA , MIAKA 50,MSAFWA,MKULIMA NA MKAZI WA IMEZU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
MAJIRA YA SAA 22:30 HRS WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA . DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI HIYO NA KULITELEKEZA GARI
ENEO LA TUKIO. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA DEREVA HUYO ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA NA TAHADHARI WAWAPO BARABARANI KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA ALIKO DEREVA HUYO
AZITOE ILI AKAMTWE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO]
MNAMO TAREHE 22.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO
MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MARRY
D/O MBUYA, MIAKA 62, KYUSA, MKULIMA KAZI WA KABWE AKIWA NA POMBE YA MOSHI
UJAZO WA LITA 9. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZINAFANYWA ILI
MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA
POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA
BHANGI.
MNAMO TAREHE 22.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:45HRS HUKO ILOMBA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LUGANO S/O
KENEDY,MIAKA 28,MNGONI,MKULIMA KAZI WA ILOMBA AKIWA NA BHANGI KETE 40 SAWA NA
GRAM 200 MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI
MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA
ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Signed By,
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
on Thursday, January 24, 2013
Post a Comment