Na: Denis Mlowe -
Iringa
Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi mkoani Iringa wanatarajia kujenga choo katika sehemu maarufu zaidi
mkoani hapa kwa biashara ya nyama ya nguruwe na vinywaji kama Vibanda vya ccm.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii Rhoda George ambaye
Katibu wa Vijana wa chama hicho mkoani hapa amesema kwamba choo
hicho
hadi kukamilika kwake
kitatumia zaidi ya shilingi milioni 3 kwa ajili ya ujenzi, kununulia vifaa na
malipo kwa mafundi.
" Kutokana na sehemu
hiyo kuongezeka kwa wateja kila siku tumeamua kujenga choo chenye matundu manne
kwa ajili ya wanaume na wanawake ili kuepusha madhara zaidi ya magonjwa
yanayoweza kujitokeza kuliko mwanzo" alisema Rhoda
aidha amesema kwamba
mara ya baada ya kukamilika watakaa pamoja na wafanyabiashara wa maeneo hayo kwa
lengo la kujadili jinsi ya kukiendesha choo hicho kuliko ilivyo sasa vyoo vyote
vinakabiliwa na uchafu kutokana na kutokuwa na matunzo jambo linalofanya mamlaka
husika kuwafungia mara kwa mara.
Sehemu hiyo ya biashara
kulikuwa hakuna vyoo vya kujitosheleza na wateja wengi walikuwa wakijisaidia
maeneo ambayo si sahihi.
Naye Naibu Meya wa
Manispaa Gervas Ndaki amewapongeza ccm vijana kwa kuweza kufanikisha ujenzi huo
kwani ni jambo la heri na kuwataka wateja waweze kukitumia kuzingatia
usafi.
"Vijana wanafanya kazi
nzuri kutokana na ilani ya ccm hivyo ni jambo la kuwapongeza sana na waangalie
maeneo mingine waweze kuboresha huduma hiyo ya vyoo kwa maeneo wanayomiliki"
alisema Ndaki
Mmoja wa wamiliki wa
mabanda hayo Thedy Ngaita alisema ni jambo zuri kwani wateja walikuwa
wanajisaidia maeneo ambayo si sahihi.
"kwa kweli iko poa sana
na tunaona ujenzi huu utatukomboa sana kuondokana na magonjwa kama UTI vyoo
vilikuwa vichafu sana na ndio chanzo cha kufungiwa biashara zetu mara kwa mara
nawapongeza kwa kweli" alisema Ngaita
Mara kwa mara maeneo
hayo yanayomilikiwa na umoja wa vijana wa ccm yalikuwa yanafungiwa kutokana na
uchafu wa vyoo na mazingira hatari kwa watumiaji na inakadiliwa zaidi ya
wafanyabiashara 100 wako maeneo ya mabanda hayo
Post a Comment