Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando (kulia) na Makamu wake, George
John.
****************************************************
CHAMA cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimepanga kufanyika mdahalo kwa wagombea wa
nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Februari 15 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa
kuendesha mdahalo huo ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA
kilichofanyika jana (Januari 23, 2012), ambapo pia kilijadili masuala mbalimbali
yahusiyo chama hicho.
Tayari
kikao kimeiagiza Sekreterieti ya TASWA ifanye maandalizi ya mdahalo huo kwa
kuzungumza na vituo vya televisheni ili uweze kuoneshwa moja kwa moja kwenye
vituo hivyo ili wananchi waweze kuwasikia wagombea hao.
TASWA
imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu kwenye uchaguzi wa TFF,
ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa wa live, ikafanya wa live
mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa, hivyo itafanya mawasiliano
na TFF ili iweze kupata msaada wa karibu kufanikisha jambo
hilo.
Tunaamini ushirikiano uliopo kati ya TFF
na TASWA utasaidia kwa namna fulani kufanikisha jambo hilo, ambapo mdahalo
utahusisha waandishi wa habari waandamizi wa michezo, wahariri wa baadhi ya
michezo na wadau wachache wa soka.
Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji
ya TASWA imemteua mwandishi wa habari mkongwe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Redio ABM, Abdallah Majura kuwa mwendeshaji wa mdahalo huo kutokana na uzoefu
wake katika masuala ya habari na mambo ya michezo.TASWA inaamini Majura ambaye
ni mwanachama wa TASWA akiwa pia amepata kuwa Katibu wa TASWA FC na Mhazini wa
TASWA ni mtu makini, asiyeyumba na mwenye kutenda haki.
Pia
Kamati ya Utendaji imesisitiza katika kikao chake kwamba uchaguzi wa TFF
haimuungi mkono mgombea yeyote na haina mpango wa kumuunga mkono mgombea yeyote,
hivyo TASWA inaonya kama kuna baadhi ya wagombea wenye ndoto za kutaka kutumia
mgongo wa TASWA kwamba chama kinawaunga mkono ili wapate mteremko kufikia
malengo yao hazitatimia.
Kama
kuna kiongozi au mwanachama wa TASWA ambaye anamuunga mkono mgombea yeyote wa
TFF, huo utakuwa msimamo wake binafsi si wa chama na kama atahusisha chama kwa
namna yoyote atakuwa anakosea na hatutasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa
katiba ya chama.
Tunawaomba waandishi wa habari za michezo
nchini kuzidisha umakini kipindi hiki cha uchaguzi wa TFF na kujiepusha na
makundi ya aina yoyote ambayo yatatia doa taaluma ya habari kwa namna yoyote
ile.
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
24/01/2012

Post a Comment