Msanii Lulu (katikati) akisubiri kusikiliza maombi yake ya dhamana kusomwa na Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke leo jijini Dar es Salaam. |
Lulu akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo. |
Kama ilivyo sikuzote ulinzi
uliimarishwa kwenye mahakama hiyo wakiwemo askari wakiume pamoja na wakike
kumlinda msanii huyo. |
Baada ya kusomewa mashart ya dhamana Lulu akiondoka huku akitokwa na machozi yanayoashiria furaha. |
Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja. Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba. (Picha na Habari Mseto Blog)
Lulu akipanga gari la magereza.
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo
Lulu akisindikizwa na askari Magereza.
Lulu akiingia katika gari la Magereza kwenda Rumande
Post a Comment