Uganda imerejesha kwa serikali ya Ireland jumla ya euro milioni 4 sawa na dola milioni 5.25 za fedha za msaada zilizogawanywa na kutumika katika malengo yasiyokusudiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Eamon Gilmore amethibitisha kufanyika kwa hatua hiyo na kusema imefuatia mazungumzo ya kina na serikali ya Uganda kwa kipindi cha miezi miwili.
Ameongeza kusema ni matumaini yake kuwa hatua kama hiyo itachangia juhudi za serikali ya Uganda kukabiliana na rushwa.
Repoti ya mwezo Oktoba mwaka jana ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Uganda ilionyesha kiasi cha euro milioni 4 za mfuko wa msaada wa Ireland zimehamishiwa katika akaunti zisizoidhinishwa katika ofisi ya Waziri Mkuu Amama Mbabazi.
Jamhuri ya Ireland ilisitisha misaada kwa Uganda mpaka hapo fedha hizo zitakaporejeshwa.
Post a Comment