Muimbaji wa Buttefly, Abubakar Katwila aka Q-Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kulisababishwa na baadhi ya watu waliochangiakumrudisha chini kimuziki na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipiitia.
Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano cha Magic FM, Qchilla alisema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo. Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.
Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliyemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.
Alisema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano P-Square na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani pekee.
Chilla ambaye kwa sasa anajiita Chichi alimalizia kwa kusema kuwa hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.
Post a Comment