Baada
ya miaka kadhaa inawezekana baadhi ya visiwa kama hivi kutoonekana kabisa
kutokana na kuendelea kuliwa kila kukicha na kupotea kabisa, na hii kwa namna
moja ama nyingine husababishwa na uharibifu wa mazingira na uharibifu wa vyanzo
vya mito, misitu nk. Visiwa hivi ni miongoni mwa Visiwa vilivyopo Bahari ya
Hindi katikati ya Dar es Salaam na Zanzibar, ambavyo vingi vionaonekana kuwa
tayari vimekwisha potea kwa kufunikwa kabisa na maji huku vingine vionekana
kuendelea kuliwa siku hadi siku.
Hiki ni
moja kati ya visiwa vidogo vilivyokwisha liwa kabisa na kufunikwa na maji,
ambapo siku za usoni hata alama hii ya kuwepoe kwa kisiwa mahala hapa
itatoweka.
Na hiki
pia ni moja kati ya visiwa vinavyoendelea kulika siku hadi
siku....
Huu ni
mmoja kati ya miamba iliyokwisha funikwa na maji
baharini.......
Hiki
nacho kama kinavyoonekana kikiwa nama kimepachikwa tu yaani kikiwa kimebaki
kimening'inia.....
Post a Comment