Wanamichezo
50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika
Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
Waombaji
ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya
Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa
akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi,
Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na
Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro
Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura,
Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na
Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na
Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na
Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya
(Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na
Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na
Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki
Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala,
Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na
Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin
Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es
Salaam).
Waombaji
wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake
utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa
Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa
Azam.
Nafasi
mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na
watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto
Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu
Mwindadi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote
zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi
Kuu.
Pia
Kamati inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za Uchaguzi,
kwani baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari. Kwa
walioanza kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika hatari ya kuenguliwa
kushiriki katika uchaguzi.
Post a Comment