Na Abdulaziz
Video.
WATU Saba akiwemo askari
polisi mmoja wameuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara,
zikiwa zimebeba sura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.
Muuguzi wa zamu hospitali
ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu
saba.
Majeruhi ambao idadi yao
haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali
bado ni tete Vurugu kubwa zilianza majira ya saa 4 asubuhi leo baada ya polisi
waliokuwa wakiendesha pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata
hivyo hoja hiyo ilihamia kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia
nyumba ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari
mawili.
Aidha vijana hao walivamia
nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM
wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika
kituo kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma moto
magari matano ya halmashauri ya wilaya.
Pia walichoma moto ofisi ya
elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya
maliasili.
Polisi kutoka maeneo
mbalimbali yandani na nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na
kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na
wananchi.
Post a Comment