 |
| Hili
ndilo kaburi ambalo Sajuki amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es
Salaam Januari 4, 2013. |
 |
| Rais Kikwete naye alikuwepo katika kumzika
Sajuki Januari 4, 2013. |
 |
| Hallooo...
hapa ndo tunakaribia kumzika mshkaji wetu
Sajuki...! |
 |
| Hapa ni maandaalizi ya mapeeema kabla jeneza
la sugu halijaletwa na mwili wa msanii huyo kuzikwa Januari 4,
2013. |
 |
| Na
mie nipishe nichukue ukumbusho wa kaburi la
Sajuki...! |
 |
| Tafakuri makini kabla ya mazishi ya Sajuki
Januari 4, 2013. |
 |
| Steve Nyerere mwenye kanzu mbele, Tino (nyuma ya
Steve) na waombolezaji wengine wakitafakari kabla mwili kufikishwa kwenye
makaburi ya Kisutu na kuzikwa jijini Dar es Salaam Januari 4,
2013. |
 |
| Tangulia
mwana... sote tuko nyuma yako Sajuki! Jotti akitafakari kabla ya mazishi ya
Sajuki Januari 4, 2013. |
 |
| Single Mtambalike 'Richie' (kushoto) naye
aliibuka 'kisheikh' kumsindikiza Sajuki Januari 4,
2013. |
 |
| Chuzi
naye alikuwepo na mtoko wake wa
Kisheikh |
 |
| Kwaheri mwanangu Sajuki... msanii nyota wa
filamu, Mzee Chillo naye alikuwapo kumzika Sajuki Januari 4,
2013. |
 |
| Hivi ni kweli umeondoka
Sajuki? Siamini! |
 |
| Mtangazaji
Benny Kinyaiya hakubaki nyuma kumsindikiza Sajuki Januari 4,
2013. |
 |
| Msanii Jimmy Mponda a.k.a Jimmy Master
alikuwa akimuaga Sajuki kwa staili
yake. |
 |
| Mhe.
Zitto Kabwe (wa pili kushoto) akitafakari jambo na wasanii na waombolezaji
wengine katika makaburi ya Kisutu kabla ya kuzikwa kwa Sajuki Januari 4,
2013. |
 |
| Kwaheri kijana wangu....! Msanii nyota wa
filamu, Mzee Magali (kulia) akionekana mwenye majonzi tele kabla ya kuzikwa kwa
mwenzao Sajuki Januari 4, 2013. (Picha zote: Shafii
Banzi) |
 |
| Said Fella (kushoto) na Chege ndani ya uzi
wajangwani pia walikuwapon |
 |
| Ni huzuni kubwa kwa kifo cha mpendwa wetu
Sajuki... Mungu amlaze pema! Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi
Azzan. |
 |
| Hapa
kabla ya kuwasili kwa mwili kwenye makaburi ya Kisutu Januari 4,
2013. |
Msanii Z Anto akiswali juu ya kaburi la Marehemu Sajuki.
King Kikii Mwana Fa na Profesa J.
Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji na Mwimbaji Linex ni miogoni mwa wasanii waliohudhuria, wengine ni pamoja na Mwana Fa, Profesa J, Mzee Kitime na King Kikii.
Rais
Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi tele wa serikali na vyama vya siasa
waliojitokeza katika mazishi ya msanii nyota wa filamu nchini, Juma Kilowoko
'Sajuki' aliyefariki juzi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuzikwa leo
katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wengine wa kisiasa
walioungana na wasanii na Watanzania wengine kibao katika kumsindikiza Sajuki
kwenye nyumba yake ya milele leo baada ya swala ya Ijumaa ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mhe. Zitto Kabwe na Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Wasanii wa filamu, muziki na watangazaji wa
redio na luninga waliokuwapo ni pamoja na Mzee Magali, Ray, Mzee Chillo, Jotti,
Richie, Cheni, Mpoki, Mac Reggan, Chegge, Ben Kinyaiya, Dulla wa East Afrika
Post a Comment