Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Muhamed akizungumza na ujumbe wa Kampuni inayo shuhulikia Ujenzi na Uchumi wa nje(ANHU)Group co,LTD ya China kulia yake ni Makamo wa Rais wa Kampuni hiyo Wang Hao,huko ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Makamo wa Rais wa Kampuni hiyo Wang Hao akionyesha baazi ya Viwanja mbali mbali vya mpira vilivyojengwa na Kampuni hiyo huko Vuga mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Bi. Asha Abdalla akiwa na Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Khalid Salum akiuliza swali kwa Makamo wa Rais wa Kampuni inayoshughulikia Ujenzi na Uchumi wa nje(ANHU)Group co,LTD ya China Wang Hao hayupo pichani huko ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Makamo wa Rais Wang Hao wa Kampuni inayoshughulikia Ujenzi na Uchumi wa nje (ANHU) Group co,LTD ya China akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Muhamed huko ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
*******
Na Zahira Bilali –Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa kuekeza katika shopping mall itakuwa kivutio kikubwa kwa watu mbali mbali na kuweza kukuza uchumi nakuondokana na umasikini nchini.
Aliyasema hayo leo huko Ofisini kwake vunga Zanzibari wakati akiwa na mazungumzo na kampuni ya (ANHU)Group co,LTD ya China.
Aidha alisema kuwa Zanzíbar ina nia ya kuekeza katika sekta ya utalii kwani sekta hiyo ndiyo inayoweza kukuza uchumi wa nchi .
Alieleza kuwa waekezaji hao wataweza kuekeza Zanzíbar mpaka waweze kufanya utafiti wa maeneo ambayo wanatarajia kuekeza ili waweze kuridhika nayo kwa biashara .
Waziri huyo amesema kuwa kampuni hiyo imeweza kuekeza sehemu Mbali Mbali za kimataifa pamoja na África Mashariki ikiwemo Zimbabwe na Mozambique
Alifahamisha kuwa katika nchi yetu ya Zanzíbar tunategemea zaidi uchumi wetu kwa njia ya utalii ikiwa wawekezaji wa kampuni hiyo wataekeza wataisaidia serikali kuengeza pato kutokana na kivutio kwa kitalii.
“Utalii ni kiungo kikubwa kwa serikali” alisema Abuod.
Alisema kuwa kampuni mbali mbali ambazo zinataka kuekeza Zanzíbar kwa kushajihisha maeneo mengine tofauti Serikali haina pingamizi kwani inaunga mkono jitihada za Serikali.
Pia alifahamisha iwapo wawekezaji wataekeza Zanzíbar wananchi watafaidika kwa kuweza kupata ajira nchini mwao .