wachezaji wa Young Africans
wakiwa mazoezin asubuhi ya leo kujiandaa na mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya
Denizlispor
Timu ya Young Africans
Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Denizlispor FC ya ligi
daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika
uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa
Antlaya.
Young Africans ambayo
imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya
kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu
ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya
Uturuki.
Kocha Mkuu wa Young
Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu
kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo
anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Baada ya kuwa na wiki moja
ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya ujerumani
mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki
na timu nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na
mazoezi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika alisema
'Brandts'
Denizlispor FC ni miongoni
mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani ambazo zimeweka kambi katika
mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la
kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji wa zamani wa
Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya Uholanzi,
mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni miongoni mwa washambuliaji wa
kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young Africans imeendelea
na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo
huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex
pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27
waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja
hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo
huo.
Athumani Idd 'Chuji' na
Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya
Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani wanaendelea na mazoezi pamoja
na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu hali ya hewa leo
haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na mda mwingi
kwa sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida
ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni
nzuri kabisa na jua linawaka mda wote.



Post a Comment