Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ziara Ya Mbunge Mwambao Wa Waziwa Nyasa Yaleta Matumaini Yaliyopotea


12 ef0b0Na : Said ng’amilo Ludewa.
WANANCHI waishio mwambao wa ziwa nyasa katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe baada ya miaka hamsini ya uhuru sasa wamepata matumaini kwa kupata miundombinu ya mawasiliano ya simu,barabara na usafiri wa majini.



Akizungumza jana katika kijiji cha Nsisi kata mpya ya Lifuma katia tarafa ya mwambao wa ziwa nyasa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe alisema mateso ya wananchi waishio mwambao huu yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Filikunjombe aliwaambia wananchi kuwa katika kipindi kifupi kijacho atahakikisha mawasiliano ya simu yanaanza ili iwe ukombozi kwa kwa mwambao huo ambapo wamekuwa wakibaki nyuma kimaendeleo kwa kukosa mawasiliano ya simu za mkononi.
Ndugu wananchi poleni na mateso mnayoendelea kuyapata ndani ya miaka hamsini ya uhuru mimi mwenzenu niliomba minara mitano ya simu serikalini nikapata mitatu na kati ya hiyo nitahakikisha minara miwili inajengwa mwambao wa ziwa nyasa kati ya katika ya Lupingu na Kilondo ili kuungana na ile ya kyela.
Filikunjombe aliwataka wananchi kuwa na subira kwani wataalamu wa minara watakuja kuangalia ni maeneo yapi mazuri yanayofaa kuijenga minara hiyo ili kupunguza kero zinazowakabili ikiwemo katika Afya ambapo wagonjwa wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika kwa kutumia simu za mkononi kuita usafiri.

Akaongeza kuwa mbali ya simu za mkononi filikunjombe aliwataka washiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuchimba barabara zinazounganisha kijiji kwa kijiji na kata kwa kata halafu yeye yuko tayari kutoa ushirikiano pamoja na serikali.
Akizungumzia barabara ya Ludewa hadi Lupingu mbunge huyo alisema tayari mkandarasi ameshaanza kazi ya ukarabati kwa kiwango cha changarawe baada ya kuipandisha hadhi na kuwa barabara ya mkoa na kupitia barabara hiyo magari makubwa yatawezo kufika ziwa nyasa.
Hata hivyo mbunge Deo akaondoa hofu iliyotanda miongoni mwa wananchi wake juu uchakavu wa meli ya Mv Songea na Mv Iringa kwa kuwaambia kuwa meli hizo ziko mbioni kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ahadi ya rais kuhusu ununuzi wa meli mpya ambayo tayari fedha za awali zimeshatolewa.
Awali wakizungumza katika mkutano wa hadhara kwa njia ya risara na kwa nyakati tofauti wananchi walimweleza mbunge wao kuwa wanakerwa sana na ratiba ya meli ya MV songea ambayo inafanya safari zake usiku badala ya mchana ambapo hulazimika kusafiri usiku na kuhatarisha maisha yao.
Akijibu maswali ya wananchi kuhusu meli hiyo kufanya safari zake usiku Filikunjombe aliwaambia kuwa atahakikisha ratiba hiyo inabadilishwa kwa sababu ajali na maafa ya meli kutembea usiku ni kubwa sana ukilinganisha na ajali za mchana.
Kuhusu suala la umeme mbunge alisema anafanya jitihada kuhakikisha umeme unafika katika kata mbili ambazo ni pamoja na Lupingu ukitokea Ludewa mjini na kata ya Makonde umeme huo ukitokea katika kata ya Mawengi unaofadhiriwa na kanisa katoliki.
Kero zingine alizokutana nazo Filikunjombe ni pamoja na wagonjwa, wanawake wajawazito na watoto kutembea umbali na kutumia muda mrefu kufuata huduma za afya katika wilaya jirani ya kyela kwa usafiri hatari wa mitumbwi na maboti yasiyo na uhakika.
Filikunjombe katika ziara yake ya siku tatu mwambao wa ziwa nyasa iliyoanza Disemba 28 hadi 31 mwaka alitoa mifuko mia moja ya saruji katika sekondari ya makonde, na vifaa vya michezo katika kila kijiji ikiwemo ng,ombe mmoja mwenye thamani ya shilingi laki tatu kila kata katika wilaya ya Ludewa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top