RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassani Mwinyi amewataka viongozi wa kidini nchini kuihami amani na utulivu inaotishiwa kuvurugwa na misukosuko ya kidini, kisiasa na kijamii inayojitokeza katika maeneo mbalimbali yanchi.
Alhaj Mwinyi alisema hayo
wakati maadhimisho ya sherehe za siku ya uzawa wa Mtume Mohamma (SWA),
yalioandaliwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaasheri, kufanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Alisema nchi hivi sasa
inapita kwenye misukosuko inayokana na vitendo hivyo na endapo viongozi wa
kidini hawatakuwa makini katika kukemea waumini wao basi huenda nchi ikaingia
kwenye matatizo ambayo hayana slahi kwa nchi.
Alhaj Mwinyi alisema mkiwa
viongozi wadini mnalo jukumu la kila mmoja wenu kutumia elimu na fursa zilizopo
kwa kuwatuliza vijana kutoingia katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwa
kisingizio cha dini.
“Tanzania inaongoza kwa
kudumisha amani, utulivu na ustaarabu kwa miaka mingi kama ingekuwa wachezaji
mpira tungesema sisi ni machampioni wa amani katika Bara la Afrika”alisema Alhaj
Mwinyi.
Alisema ni wajibu wa
Masheikh hao kusimamia na kulinda amani na utulivu uendelee kuwepo ili kila
muumini aweze kufanya ibada, kwenda msikitini na kufanya shughuli nyingine za
maendeleo kwa maslahi ya nchi.
Aliongeza kuwa hakuna haja
ya kufikishana mahala kuwa kila mmoja anakuwa na wasiwasi wa maisha yake kitendo
ambacho kinaenda kinyume na mafundisho ya Mtume Mohamad
(SWA).
“Tanzania ni nchi kongwe na
haikuanza leo pia ni sawa na gunia ambalo limekusanya watu wengi wa dini
mbalimbali na wasio na dini hivyo ni vema watu wakajenga ustaarabu wa
kuvumiliana”alisema Alhaj Mwinyi.
Alhaj Mwinyi alisema wajibu
wa Waislam ni kuhakikisha wanaishi kwa amani na watu wengine ambao
hawajawaingilia na kutaka kuwafuta katika nchi hii.
Vilevile ieleweke wazi kuwa
hakuna anaweza kumfuta mwenzake katika kile anachokiamini hivyo ni vema kila mtu
akajifunza kumvumilia mwingine.
Alisema kubwa ni kla mmoja
kujizuia kumuingilia mwingine kwenye dini yake, kazi hiyo hakuna mwingine wa
kuifanya bali ni Masheikh hao.
Aliwaasa Masheikh hao
kuacha kushabikia mambo madogo ambako ushabibiki ukiendekezwa iko siku unaweza
kuvuruga amani ya nchi hii.
Post a Comment