Waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda wamefunga barabara kwa muda mkoani morogoro.
Waendesha pikipiki hao
wamefunga barabaraya kutokea mjini kuelekea kituo
kukuu cha mabasi msavu eneo la masika wakipinga utaratibu mbovu unaotumiwa na
mamlaka ya kukusanya kodi mkoa wa morogoro (TRA) Wa kuwakamata waendesha
bodaboda hao bila utaratibu,Akisumulia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha
waendesha bodaboda hao amesema TRA wameanza utaraibu wa kuwakimbiza waendesha
pikipiki hao kwa kutumia magari jambo ambalo ni hatari kwa usalama
wao.
Akiendelea amesema pia
wamekuwa wakiwakamata kwa vurugu na bugudha kubwa bila kujali wapo waliolipa
kodi na ambao hawajalipa kodi.
Moto uliowashwa na
waendesha bodaboda hao waliofunga barabara mkoani morogoro kwa kuchoma matairi,
kupanga magogo,na mawe barabarani kwa lengo la kuipinga uwonevu unaofanywa na
mamlaka ya kukusanya mapatoya kukusanya mapato mkoa
wa morogoro dhidi yao.Moto huo ukiendelea kuwaka kabla ya kudhibitiwa na jeshi la polisi mchana huu
Moto huo ukizimwa na kikosi cha zimamoto mkoa wa morogoro baada ya kufuka eneo la tukio
wakazi wa morogoro wakiwa wamesimama kando ya barabara hiyo kushuhudia tukio hilo mchana huu mjini morogoro
Mkuu wa kituo cha polisi morogoro mjini akiwa eneo la tukio kuhakikisha usalama na amani unakuwepo baada ya kufanikiwa kudhibiti tukio hilo
Post a Comment