BAADHI ya wakazi wa maeneo ya Mafisa mkoani hapa wamekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha leo jioni,
Mbali na kuezua nyumba hizo pia upepo huo uliangusha miti mirefu,taa za barabarani na mabango marefu ya matangazo ya makampuni ya simu ya vodacom na tigo
Miongoni mwa mabango hayo ni bango kubwa la vodacom ambalo liliwekwa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu katikati ya geti kuu la kutokea mabasi eneo ambalo pia madereva wa boda boda huegesha pikipiki zao chini ya bango hilo.
" Ni mungu tu ametunusulu na kifo wakati bango hili linaanguka sisi tulikuwa hapa chini tukisubiri abiria kwa bahati tuliwahi kustuka,na kukimbia mwenzetu mmoja kwenye heka heka ya kukimbia aliiacha pikipiki yake ambayo aliangukiwa na bango hili na kuhalibika vibaya"alisema mmoja wa mabareva hao wa boda boda aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Samwel
Hii ni mara ya pili kwa bango la kampuni hizo kuanguka ambapo mara ya kwanza takribani miaka miwili iliyopita bango la tigo lililowekwa katikati ya stendi ya daladala lilianguka na kuharibu daladala mbili ambazo kwa bahati zilikuwa hazina watu ingawa zenyewe zilihalibika vibaya baada ya kuanguliwa na bango hilo.
Pia upepo huo uliovuma jana kutoka upande wa kaskazini ya mji wa Morogoro uliezua nyumba za watu na kuangusha miti mirefu ambapo hadi mtandao huu unakwenda hewani takribani nyumba 15 ziliezuliwa mapaa hali iliyosababisha wakazi wa nyumba hizo kukosa mahali pa kuishi.
Post a Comment