Kikundi cha chipukizi wa Umoja wa Vijana na wahasishaji kutoka katika Mkoa wa Dodoma, wakiwa wanahamasisha na kuchangamsha wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa. |
|
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa Ndg Sadifa ametengua uteuzi wa wajumbe wa baraza ambao
alikuwa amewateua Ndg Paul makonda pamoja na Msaraka , Makonda katolewa
kikaoni sasa hivi kwa kuwa uteuzi umetenguliwa kaambiwa sio mjumbe tena
awapishe kikaoni!! UVCCM tutafika kweli , guy hii sio bure tumerogwa
Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) unafanya kikao chake cha kwanza
cha Baraza Kuu la Umoja huo, ambapo ajenda mbalimbali zitajadiliwa
ikiwemo tathmini juu ya Hali ya Vijana na Siasa Nchini, lakini pia
tathmini ya sehemu ya mkakati wa maamuzi ya Mkutano Mkuu ikiwemo
mikakati ya kuimarisha Chipukizi na Uhamasishaji.
Pamoja na hayo, kutajadiliwa pia mikakati ya kiuchumi ya kuiwezesha jumuiya ya Umoja wa Vijana kujitegemea kiuchumi kwa kuweka mipango imara ya uzalishaji ili kukuza mapato ya jumuiya. Kikao kitajadili miradi iliyopo na muendelezo wake lakini pia kutafakari juu ya kuanzisha miradi mipya ya jumuiya hiyo.
Kikao hicho kitafanya Uteuzi wa Baraza la wadhamini wa UVCCM pamoja na Kamati ya utekelezaji, kisha kitamalizika kwa semina kwa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa juu ya wajibu na majukumu ya wajumbe wa Baraza na kukumbushana juu ya majukumu na wajibu wa jumuiya ya UVCCM katika kuimarisha Uhai wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya shina hadi Taifa

Post a Comment