Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BENKI YA NMB YATAHADHARISHA WATEJA WAKE


DAR ES SALAAM, Tanzania

MENEJIMENTI ya NMB imewaonya wateja wake na umma kwa ujumla kuwa imegundua kwamba kuna taasisi inayojitambulisha kama Tanzania Loans Society inadai kuwa mshirika wa benki hiyo katika kutoa huduma za kibenki.

Taasisi hiyo imedaiwa kuwa kwa kutumia mtandao wake wa intaneti imekuwa ikijinasibu kutoa mikopo ambayo fedha zake zimeidhinishwa na NMB kupitia kwa mameneja wa matawi.

Aidha, Tanzania Loan Society pia inadaiwa kueleza kwamba fomu za maombi ya mkopo na malipo ya usajili vinaweza kulipwa kwa kutumia namba ya simu ya mkononi.

Menejimenti ya NMB imezidi kuwatahadharisha wateja wake na umma kwa ujumla kwamba haina ushirika au makubaliano yoyote na taasisi hiyo katika shughuli zake.

Imeongeza kuwa, NMB hutoa mikopo yake kupitia matawi yake tu, na hakuna namna yoyote ambayo inaweza kusababisha gharama za maombi ya mikopo au mikopo kutolewa kupitia simu za mkononi.

Menejimenti hiyo imesisitiza kuwataka wateja na umma kwa ujumla kutojihusisha na taasisi hiyo katika shughuli yoyote inayoihusu Benki ya NMB na kwamba haitahusika kwa namna yoyote na matatizo yatakayojitokeza

 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top