Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Enoch Osei-Safo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa halfa fupi ya kukabidhi zawadi ya gari mpya aina ya Hyundai Tucson ix35 kwa mshindi wa Shindano lililokuwa likiendeshwa na benki hiyo la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka kutoka Tegeta, Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa sekta ya Umma Ecobank Ndabu Swere na Kutoka kushoto ni mshindi wa Shindano la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka, Mkuu wa Bidhaa na Masoko Ecobank Andrew Lyimo, Mkuu wa Domestic Banking Joyce Malai.

Mkuu wa Domestic Banking Joyce Malai akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) wakati wa halfa ya kukabidhi gari kwa mshindi wa shindano la shinda Babkubwa na Ecobank. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Enoch Osei-Safo na kulia ni Mkuu wa sekta ya Umma Ecobank Ndabu Swere.

Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Enoch Osei-Safo (katikati) akikabidhi funguo ya gari kwa mshindi wa Shindano lililokuwa kiendeshwa na benki hiyo kwa wateja wake la shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka (kulia) kutoka Tegeta, jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni Mkuu wa Domestic Banking Joyce Malai.


Mshindi wa shindano la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka akijaribu gari lake baada ya kukabidhiwa rasmi leo jijini Dar huku akitoa tabasamu bashasha kuonyesha furaha isiyonakifani. Anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni Mkuu wa Domestic Banking Joyce Malai.
Mshindi wa shindano la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka akijiandaa kuzungumza na vyombo vya habari ambapo alihamasisha wananchi kujiunga na benki hiyo kupata huduma bora kwani nao siku moja wanaweza kubahatika kama yeye.
Shindano la Shinda Babkubwa na Ecobank leo limekamilika kwa makabidhiano ya tuzo kuu ya gari mpya aina ya Hyundai Tucson ix35 kwa mshindi Bw. Ipyana Mwakasaka kutoka Tegeta, Dar es Salaam.
“Nimefurahi sana kuwa mshindi wa tuzo hili la gari jipya zuri ambalo litatusaidia sana mimi na familia yangu katika kutatua shida za usafiri” alisema Bw. Ipyana.”Ecobank imeonyesha na inazidi kutimiza ahadi yake ya kuridhisha wateja wake pamoja na huduma kwa wateja ya hali ya juu katika matawi yake. Pia mitandao ya Ecobank ya e-banking na ATM zimeturahisishia uendeshaji wa akauti zetu kwa njia iliyo salama zaidi” aliongeza.
Shindano hili lililowalenga wateja binafsi, wanabiashara na kampuni ndogondogo na za kiasi cha kati, lilianza Juni 2012 na kuendelea hadi mwisho wa mwaka 2012.
Mkuu wa Bidhaa na Masoko Ecobank Andrew Lyimo Tanzania amesema wateja waliokuwa na amana ya 100,000 kuendelea walishiriki kwenya droo hii, ambapo kila mwezi palikuwa na washindi wa iPads, Laptops, vocha na zawadi yenye thamani ya shilingi 500,000 na safari kwenda Zanzibar na Ushelisheli,.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Enoch Osei-Safo anasena Tanzania Hii ni moja kati ya mikakati mingi kwa ajili ya Ecobank kukuza ushirikishwaji wa kifedha kwa Watanzania kwa kutoa huduma nafuu na rahisi ya ufumbuzi wa fedha kwa wanajamii na wafanyabiashara. Lengo letu ni kutoa ufumbuzi wa kifedha ambao umehakikisha mafanikio kwa wa Afrika kupitia mtandao wetu mkubwa Afrika nzima, hatua ambayo imedhibitika kukuza ustawi wa kiuchumi,
Ecobank Tanzania ina nia ya kueneza elimu ya kifedha na kuelimisha umma juu ya faida na fursa zilizopo katika sekta ya benki. Katika miezi michache ijayo, sisi tutazindua mipango ya kukuza zaidi ushirikishwaji wa fedha kwa waTanzania ili kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawajafikiwa na huduma za benki” Enoch alielezea. Hii inakwenda sambamba na mkakati wa kitaifa kwa ajili ya kukuza uchumi ili kuwawezesha wananchi kupata faida na fursa katika Tanzania, Afrika na dunia nzima.
Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.ecobank.com