Loading...
BREAKING NEWS: PADRI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ZANZIBAR
Padre wa Kanisa la Katoliki la parokia ya Minara Miwili lililopo mji mkongwe, Padri Evarist Mushi amefariki Dunia baada ya kupigwa risasi utosini na watu wasiojulikana. Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi hii kwenye kanisa la Mt. Theresia na akiwa eneo la Mtoni alisimamisha na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga risasi utosini na kufariki papo kwa papo ambapo mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali kuu ya Zanzibar iliyopo Mnazi Mmoja.
Hili ni tukio la pili kutoka la kudhuliwa kwa Mapadri huko Zanzibar ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mpaka sasa hakuna askari hata mmoja aliyefika eneo la tukio.
............... endelea kuwa na NDGSHILATU Blog mahala popote na wakati wowote tutakuletea picha za tukio hilo la kusikitisha .........
Post a Comment