Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HABARI KUTOKA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA

IMG_0445
JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKITA) limesema kuwa katika muongozo wa Tume juu ya muundo na utaratibu wa kupata wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Asasi unamapungufu katika baadhi ya vipengele. Akizungumza Dar es Salaam leo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Deus Kibamba alitaja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni Madiwani wasiwe wajumbe wa moja kwa moja wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,maoni juu ya mwongozo yametolewa na watu wachache,sifa za watakaochaguliwa kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya zinamapungufu.
Deus alisema ili kupanua wigo wa Demokrasia na kuepuka mgongano wa kimaslahi ,Jukwaa limependekeza kuwa Madiwani wasiei wajumbe wa moja kwa moja kwa nyadhifa zo,katika mabaraza ya Wilaya ,Ngazi ay Serikali za Mitaa na badala yake wanaotaka kuwa wajumbe wajumbe waombe ridhaa mpya ya wananchi ili kuweza kuchaguliwa katika mabaraza hayo.
Alisema kuwa sababu za kutoa mapendekezo hayo kuwa madiwani wasingie kwa nafasi zao kwasababu Madiwani walichaguliwa kwa ajili ya kazi ya kuwawakilisha wananchi katika ngazi ya mabaraza ya Madiwani ya Wilaya ,manispaa ,miji na majiji na si kwa ajili ya mabaraza ya katiba.
Alieleza wawakilishi wanne watakaochaguliwa kutoka kila kijiji na kata watakuwa na mamlaka stahili ya kuwakilisha wananchi kama ilivyo kwa madiwani katika mabaraza ya madiwani.

Alifafanua kuwa uwakilishi wa madiwani utaleta mgongano wa itikadi za vyama vilivyowaweka madiwani hao madarakani hivyo kuleta msigano kwenye mchakato wa mabaraza ya katiba.
‘’kama kuna ulazima wa madiwani kuingia katika mabaraza hayo madiwani husika waombe ridhaa ya kuingia katika mabarza kwa kupigiwa kura kupitia kijiji husika’’alisema Deus
Aidha alisema kuingia kwao moja kwa moja kutaweka mazoea mabaya kwa vyombo vitavyoundwa siku za badae katika mchakato huo wa katiba mpya pamoaj na kuingia kwao kunaleta utata juu ya endapo wabunge ambao nao ni madiwani kwa nyadhifa zao kama wabunge ,watashiriki mabaraza ya katiba au hawatashiriki .
Sababu nyingine kuwa madiwani jukumu lao ni usimamamizi wa shughuli za maendeleo na masuala ya uongozi na siasa katika kila kata hivyo wanashauriwa madiwani wabaki hivyo ili wasaidie wanapohitaji ka katika majukumu hayo ya kila siku kuliko wakiwa wajumbe katika mabaraza ya katiba.
Alisema walibaini kuwa muongozo unatoa madaraka yasiyo na ukomo kwa watendaji wa vijiji na masheha katika kuratibu zoezi la upatikanaji wa wajumbe wa mabaraza ya katiba.
Alisema Pamoja na mapendekezo hayo muongozo utamke bayaana namana madaraka hayo yanavyodhibitiwa kwa kutamka watu wanaoweza kumzuia asiweke upendeleo kwa baadhi ay watu waliopendekezwa kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba.
Hatahivyo alisema endapo mapungufu aytafanyiwa kazi Muongozo huo utakuwa ni mfano wa kuigwa na utafanya kazi ya mabaraza ya katiba yawe ya wazi na shirikishi kwa kiwango kikubwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top