* Masheikh wengine wawili wasakwa, pamoja na Askof mmoja.
POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa
Msikiti wa Ijumaa Imaam Hamza, huku likitangaza kuwasaka masheikh wawili
wengine pamoja na Askofu (majina yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi
wa kidini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest
Mangu alisema Imamu huyo wa msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya kubainika
kwamba wanahusika na usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa zikihamasisha
vurugu pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala la
kuchinja.
Kwa upande wake Askofu Mpemba wa Kanisa la
Tanzania Field Evangelist yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa video
(DVD) yenye jina la ‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili wanasakwa kwa
kuhusika na uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD) zenye majina ya ‘Unafiki
katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Uadui wa
Makafiri’.
Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata
Taifa kufuatia hatua ya Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua
madaraka Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata utaratibu
Post a Comment