Mulugo aliliambia NIPASHE
kuwa wizara inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize
kufanya kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi hao.
“Kwa sasa siwezi nikasema chochote kwani tume imeundwa ili
kulifanyia kazi jambo hilo, hivyo tunasubiri wamalize kufanya kazi yao ndipo
tutatoa kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi walio feli kama ni kurudia tena
mtihani au la,” alisema Mulugo.
Alitoa ufafanuzi huo baada
ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya
muda mfupi kwa vijana wote waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo
wanaaoweza kusaidiwa kuendelea na elimu ya cheti.
Msambatavangu alitoa uamuzi
huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha
Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana kutoa mafunzo hayo
yatakayo anza Machi mwaka huu.
Mulogo alisema kuwa ni wazo
lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi ambao ni kama wamekumbwa na tatizo
kwa sasa, hivyo anacho kifanya Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote na
anafanya kama raia mwema aliyeguswa na matokeo hayo
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment